1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya wapelelezi yasema Iran si tishio kubwa kinyuklia

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWgL

Mradi wa nyuklia wa Iran si tishio kubwa kama serikali ya Rais Bush inavyosema.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa upelelezi wa Marekani.Mshauri wa serikali ya Marekani kuhusu masuala ya usalama,Steven Hadley amesema,ripoti hiyo yaonyesha kuwa sera za Rais wa Marekani George W.Bush kuelekea Tehran zimefanikiwa. Akaongezea kuwa Iran ilisitisha mradi wake wa kutengeneza bomu la atomu katika mwaka 2003.

Hata hivyo wataalamu wa upelelezi wa Marekani waliotayarisha ripoti hiyo wanaamini kuwa Iran imejiachia uwezekano wa kuanzisha upya mradi wake wa silaha za nyuklia.

Iran inashinikzwa kusita kurutubisha madini ya uranium,ikihofiwa kuwa ina mpango wa kutengeneza silaha ya nyuklia kwa siri.Tehran lakini mara kwa mara imekanusha madai hayo na kusema,mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.