1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH : Mkutano wa viongozi wa OPEC wafanyika Saudia

17 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImB

Shirika la nchi zenye kuzalisha mafuta kwa wingi duniani OPEC litaunga mkono mapambano dhidi ya kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani mwishoni mwa juma hili na imeyakinisha ahadi yake ya kutuliza na kuzifanya bei za mafuta kuwa na ushindani .

Kwa mujibu wa rasimu ya azimio ya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa OPEC shirika hilo linashirikiana wasi wasi na jumuiya ya kimataifa kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto za muda mrefu na kwamba shirika hilo pia linataka kuwepo utulivu kwenye masoko nishati duniani.

Viongozi wa nchi wanachama wa OPEC wanaanza kukutana leo hii katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh huku bei ya mafuta ya petroli kwa pipa ikikaribiwa kufikia dola 100.