1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH : Putin ziarani Mashariki ya Kati

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSr

Rais Vladimir Putin wa Urusi leo hii amekubali kuisaidia Saudi Arabia kuzalisha nishati ya nuklea na kuahidi kuendeleza ushirikiano na ulimwengi wa Kiislam katika ziara yake ya kwanza nchini Saudi Arabia ambayo ni rafiki muhimu wa Marekani.

Putin ametaja maendeleo ya nishati ya atomu kuwa mojawapo ya fani muhimu ya ushirikiano kati ya Urusi na Saudi Arabia.

Pendekezo hilo la Putin akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya Mashariki ya Kati kukuza ushirikiano wa kijeshi na nishati na washirika wa jadi wa Marekani inafuatia tangazo na mataifa ya kitajiri ya Kiarabu ya Ghuba miezi miwili iliopita kutaka kutafuta teknolojia ya nishati ya nuklea.

Baadae leo hii Putin anatazamiwa kuelekea Qatar makao makuu ya vikosi vya Marekani huko Mashariki ya Kati.

Pia anatazamiwa kwenda Jordan ambapo atakutana na Mfalme Abadullah na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina.