1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Viongozi wa Kiarabu wakubali kufufua mchakato wa amani

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEN

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Nchi za Kiarabu umemalizika katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.Viongozi katika mkutano huo wameidhinisha kufufua mchakato wa amani,ili kumaliza mgogoro wa Israel na Wapalestina.Mpango huo ulipendekezwa kwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita.Israel wakati huo,ilipinga masharti ya kimsingi yaliyotolewa na Waarabu kuwa Israel irejee kwenye mipaka ya kabla ya vita vya mwaka 1967,Jerusalem ya Mashariki iwe katika taifa la Palestina litakaloundwa na wakimbizi wa Kipalestina warejee katika lile eneo ambalo hivi sasa ni Israel. Katika tamko la pamoja la kufunga mkutano wa siku mbili,viongozi wa nchi za Kiarabu vile vile wameonya dhidi ya mashindano ya kumiliki silaha za nyuklia katika kanda hiyo,hapo zikimaanishwa Israel na Iran.