1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robben mchezaji bora wa nusu ya kwanza ya msimu

Admin.WagnerD5 Januari 2015

Mchezaji wa Bayern Munich Arjen Robben ametajwa kuwa mchezaji bora wa mzunguko wa kwanza wa msimu wa Bundesliga, katika kura iliyopigwa na wachezaji 240 wa Bundesliga.

https://p.dw.com/p/1EFGQ
Fußball 1. Bundesliga 1. FSV Mainz 05 vs. FC Bayern München
Picha: Reuters/R. Orlowski

Robben alitawala kura hiyo, iliyoendeshwa na jarida la michezo la Kicker na kutangazwa leo Jumatatu, akipata asilimia 46.7, akiwatangulia mchezaji wa kati wa Wolfsburg Kevin de Bruyne pamoja na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Alexander Meier.

Katika uchaguzi mwingine Manuel Neuer wa Bayern Munich ametajwa kama mlinda mlango bora, Karim Bellarbi wa Leverkusen ameteuliwa kama mchezaji chipukizi bora , na Markus Weinzierl wa Augsburg amekuwa kocha bora wa mzunguko wa kwanza.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre , afpe , dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga