1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROM: Rais Bush akutana na Papa Benedikt XVI

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtM

Rais George W.Bush wa Marekani anafanya ziara fupi nchini Italia.Mbali na kuonana na Rais Napolitano na Waziri Mkuu Prodi wa Italia,Bush vile vile ana mkutano wa faragha pamoja na Papa Benedekit wa 16.Kwa mujibu wa Vatikan,Papa atagusia vita vya Iraq,ambavyo vilipingwa na mtangulizi wake marehemu Papa Yohanna Paulo wa Pili.Kwa upande mwingine,Vatikan imesifu msimamo wa Bush wa kupinga kitendo cha kutoa mimba. Wakati huo huo,polisi wamejitayarisha kwa maandamano ya wapinzani wa utandawazi pamoja na makundi ya sera za mrego wa kushoto,ambayo hupinga vita vya Iraq,ambayo imekaliwa na Marekani.Waziri Mkuu Prodi ametoa mwito kwa wanachama wa serikali yake ya mseto mwa vyama vingi,kujiepusha na maandamano hayo,lakini baadhi ya wajumbe wanatazamia kushiriki katika maandamano.Hapo kabla,Bush alipitia Poland baada ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la mataifa manane tajiri yalioendelea kiviwanda G8 mjini Heiligendamm kaskazini mwa Ujerumani.