1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Italia yataka hukumu ya kifo ipigwe marufuku duniani

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdl

Waziri mkuu wa Italia, Romano Prodi amesema nchi yake itataka hukumu ya kifo ipigwe marufu duniani kote. Italia itawasilisha pendekezo lake kwa Umoja wa Mataifa baada ya kuchukua kiti cha muda katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Italia katika umoja huo, Marcello Spatafora tayari amelitaka baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuijadili tena hukumu ya kifo. Italia imewahi mara mbili kuwasilisha pendekezo la kufutiliwa mbali kwa hukumu ya kifo kwa umoja wa mataifa.

Wabunge wa Italia katika serikali na upande wa upinzani wameeleza kutofurahishwa kwao na kunyongwa kwa rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein.