1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:Maiti za Wahamiaji haramu 14 zaelea baharini

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYu

Miili ya wahamiaji haramu 14 imepatikana kwenye pwani ya visiwa vilivyo kati ya Malta na Tunisia.Kulingana na maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Italia miili hiyo bado ina marungu ya kujilinda na inaelea majini.Wanamaji wa Italia waliiona miili hiyo katika eneo lililo na umbali wa takriban kilomita 90 kusini mwa kisiwa cha Lampedusa huku mitumbwi myengine ikielekea huko.

Polisi katika eneo hilo wanaendelea kuokoa miili hiyo. Eneo la kusini mwa Italia na Malta hukabiliwa na tatizo la wahamiaji haramu wengi wao kutoka Kaskazini mwa Afrika.Wahamiaji hao wanajaribu kufika Ulaya kwa kutumia mitumbwi midogo.Zaidi ya wahamiaji 100 haramu walionekana hapo jana na kuzuiliwa katika kisiwa cha Lampedusa.

Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR watu 77 walifariki na wengine 133 kupotea mwezi Juni walipojaribu kuvuka mlango wa bahari wa Sicily unaotenganisha nchi ya Italia na eneo la kaskazini mwa Bara la Afrika.