1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Romney, Santorum bega kwa bega

7 Machi 2012

Mgombea mwenye matumaini ya kuwania kiti cha urais nchini Marekani kwa tekiti ya chama cha Republican Mitt Romney amepata ushindi muhimu katika majimbo matatu muhimu,katika kile kinachojulikana kama Super Tuesday.

https://p.dw.com/p/14GAV
Republican presidential candidate and former Massachusetts Governor Mitt Romney speaks at a town hall meeting campaign stop at USAeroteam in Dayton, Ohio March 3, 2012. REUTERS/Brian Snyder (UNITED STATES - Tags: POLITICS ELECTIONS) // eingestellt von se
Mgombea anayeongoza kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa na chama cha Republican Mitt Romney,Picha: Reuters

Gavana wa zamani wa jimbo la Massachusetts Mitt Romney ameshinda majimbo ya Virginia, Vermont, Massachusetts na jimbo muhimu la Ohio, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, baada ya vituo vya kupigia kura katika majimbo hayo kufungwa , katika mpambano mkali wa kuwania uteuzi kwa tikiti ya chama cha Republican katika uchaguzi wa rais hapo Novemba mwaka huu dhidi ya rais Barack Obama kutoka chama cha Democratic.

Gingrich aambulia

Spika wa zamani wa baraza la wawakilishi nchini Marekani Newt Gingrich , anahitaji ushindi kuweza kurejea katika njia ya kuwania tikiti hiyo ya chama cha Republican , ambapo ameshinda kwa kishindo katika jimbo anakotoka la Georgia, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali , Gingrich amepata asilimia 45 katika jimbo la Georgia, ikilinganishwa na asilimia 26 alizopata Mitt Romney na asilimia 20 kwa seneta wa zamani kutoka jimbo la Pennsylvania Rick Santorum.

Sen. Rick Santorum, R-Pa., walks to a news conference in downtown Pittsburgh on Monday, July 11, 2005. A hearing officer has sided with U.S. Sen. Rick Santorum in a dispute over whether a Pennsylvania school district can get back tax money it paid for Santorum's children to attend an Internet-based charter school while living in Virginia. (AP Photo/Keith Srakocic)
Mgombea anayemkaribia Romney , Rick SantorumPicha: AP

Romney mwenye umri wa miaka 64 anamatumaini ya kushinda mengi kati ya majimbo hayo kumi ambayo yamepiga kura jana Jumanne na kuondoa shaka zilizopo kuwa yeye ni mgombea bora kabisa kwa ajili ya uchaguzi wa hapo Novemba mwaka huu dhidi ya Barack Obama.

Kazi bado pevu

Lakini hata baada ya uchaguzi uliofanyika jana Jumanne bado njia ni ndefu katika mpambano huo wa jimbo kwa jimbo wa uteuzi wa chama cha Republican ambapo hatimaye mgombea wa chama hicho atateuliwa.

Mbali na Mitt Romney kupata ushindi wa majimbo matatu muhimu, lakini mgombea mwingine Rick Santorum ameshinda pia katika majimbo matatu muhimu ya Oklahoma ,Tennesseee na Virginia.

Wagombea wanaofuatia nyuma ya Mitt Romney na Rick Santorum, ni Gingrich na Ron Paul , wote wakiwa na matumaini ya kupata sehemu yao ya kura za wajumbe wanaohitajika ili kuweza kupata kuteuliwa.

Republican presidential candidate former House Speaker Newt Gingrich speaks during a campaign stop, Friday, Dec. 23, 2011, in Columbia, S.C. (AP Photo/Rainier Ehrhardt)
Spika wa zamani wa baraza la wawakilishi Newt GingrichPicha: AP

Obama awatakia heri wagombea

President Barack Obama speaks during a news conference in the James Brady Press Briefing Room of the White House in Washington, Tuesday, March 6, 2012. (Foto:Charles Dharapak/AP/dapd)
Rais wa Marekani Barack Obama katika mkutano na waandishi habari March 6,2012.Picha: dapd

Rais Barack Obama nae ameweka mtazamo wake katika kinyang'anyiro hicho cha chama cha Republican mapema jana Jumanne katika mkutano na waandishi habari katika Ikulu ya Marekani ya White House. Kitu gani unataka kumwambia Romney , Obama aliulizwa saa kadha kabla ya vituo vya uchaguzi kufungwa. Kila la kheri , amesema akitabasamu, na kusababisha kicheko kutoka kwa waandishi habari.

Mwandishi : Sekione Kitojo /dpae/afpe/rtre