1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK: maandamano zaidi yafanyika

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuj

Maandamano mengine yamefanyika katika mji wa Rostock ulio mashariki mwa Ujerumani huku zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kuanza mkutano wa kilele wa viongozi kutoka nchi nane zilizostawi kiviwanda G8 unaotarajiwa kufanyika katika mji wa Heiligendamm.

Polisi imearifu kuwa zaidi ya waandamanaji 1000 walishiriki katika maandamano hayo kupinga sheria za uhamiaji katika nchi wanachama wa kundi la G8.

Wakati huo huo wanaharakati wanaopinga utandawazi wamekata rufaa katika mahakama ya juu nchini Ujerumani dhidi ya amri ya kupiga marufuku mandamano karibu na maeneo ya mji wa Heiligindamm kutakapo fanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za G8.