1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK:Polisi 50 wajeruhiwa na wapinzani wa utandawazi

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBud

Wandamanaji wamepambana na polisi wa kupambana na ghasia, katika mji wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani wa Rostock, mnamo wakati ambapo wakuu wa nchi za G8 wanajiandaa kwa mkutano wao wa kilele kesho huko Hailegendam.

Kiasi cha polisi 50 wamejeruhiwa, ambapo wandamanaji 66 wamekamatwa.

Hata hivyo ghasia hizo ni tofauti na za jumamosi iliyopita, ambapo kiasi cha watu elfu moja wakiwemo polisi mia nne walijeruhiwa.

Mkutano huo wa siku tatu wa wakuu wa nchi nane zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani unatarajiwa kuanza kesho.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alielezea matumaini yake kuhusu mkutano huo.