1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruksa rais mteule wa Korea Kusini kuchunguzwa

10 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cnev

SEOUL

Mahkama ya Katiba ya Korea Kusini imepitisha hukumu kwamba jopo maalum lenye kuchunguza madai ya hujuma dhidi ya Rais mteule Myung-bak Lee linaweza kuendelea na uchunguzi wake juu ya kwamba sehemu ya mchakato huo ni kinyume na katiba.

Lee ambaye ni meya wa zamani wa Seoul na mkuu wa kampuni ya ujenzi amekuwa chini ya uchunguzi kwa madai ya kuhusika kwake katika kampuni inayoshukiwa kuwadanganya wawekezaji.