1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rumsfeld asifiwa na rais Bush kwa mchango wake nchini Irak

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCis

Washington:

Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld ameagwa kwa heshima zote za kijeshi baada ya kuongoza wizara hiyo kwa miaka sita.Rais George W. Bush amemshukuru na kumsifu mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 74 hasa kutokana na mchango wake kaatika siasa ya Marekani kuelekea Irak.Chini ya uongozi wake,jeshi la Marekani limeweza kuwasaidia wairak,tunanukuu-kutia njiani mfumo wa kidemokrasi unaoambatana katiba-mwisho wa kumnukuu rais George W. Bush.Donald Rumsfeld ameitumia fursa hiyo kupinga kurejeshwa nyumbani wanajeshi wa Marekani kutoka Irak.Robert Gates,kiongozi wa zamani wa shirika la upelelezi la Marekani CIA atakabidhiwa rasmi wadhifa wa waziri wa ulinzi,jumatatu ijayo.Rumsfeld alijiuzulu kufuatia ushindi wa wademocrats katika uchaguzi wa mwezi uliopita.