1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Russia na Misri za tia saini makubaliano ya nishati ya Kinyuklia

26 Machi 2008

Hatimaye Russia na Misri zimetia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya nishati ya nuklia.

https://p.dw.com/p/DV1a
Rais Vladimir Putin akizungumza katika Mkutano wa chama tawala mjini Moscow, Jumatatu, Oct. 1, 2007.Picha: AP

Makubaliano hayo yanafuatia mazungumzo ya miaka mingi ambayo yamekuwa yakifanywa na wanadiplomasia wa pande zote mbili.

Makubaliano hayo yalisainiwa wakati wa ziara ya rais wa Misri Hosni Mubarak nchini Russia.

Ujenzi wa kinu cha kwanza cha kinyuklia unatarajiwa kutangazwa mwaka huu, mradi huo unakadiliwa kugharimu zaidi ya dola mbili.

Misri pia inapanga kujenga vinu vingine vitatu vya Kinyuklia ili kukidhi mahitaji yake ya nishati hiyo na kuongeza vyanzo vyake ambavyo vitaweza kuhifadhi Haidrokaboni kwa muda mrefu..

Russia inatafuta njia za kuboresha zaidi sekta ya Teknolojia ili kupunguza utegemezi wa kuagiza mafuta na gesi na ndiyo maana imekuwa na hamu ya kusainiwa kwa makubaliano hayo ili kujenga kinu cha Nyuklia nchini Misri.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkuu wa Shirika la Taifa la nishati ya Nyuklia lijulikanalo kama Rosatom, Sergey Kiriyenko na Waziri wa Nishati wa Misri Hassan Younes.

Mpango huo pia unalenga kutoa mafunzo binafsi juu ya utumiaji wa vifaa vya Kinyuklia yatakayofanyika nchini Misri na usambazaji wa mafuta katika nchi hiyo.

Kampuni ya Atomstroyexport ambayo inasimamia shughuli zote za utengenezaji wa Vifaa vya kuzalisha umeme kwa nguvu za nyuklia, hivi karibuni ilitengeneza vinu vitano vya nishati hiyo katika nchi za China, India na Iran ambavyo viligharimu kiasi cha dola bilioni nne nukta tano.

Kampuni hiyo pia imepata kandarasi ya kutengeneza vinu hivyo katika mji wa Belene nchini Bulgaria wakati huohuo kukiwa na mazungumzo ya kujenga vinu kama hivyo huko Morocco, Vietnam na Afrika Kusini.

Msemaji katika shirikisho la Wakala wa Kinyuklia ambayo inaongoza mpango wa Taifa wa Kinyuklia njini na katika nchi za nje, ameliambia Shirika la habari la IPS, mara tu baada ya kusainiwa makubaliano hayo kwamba Russia inajiandaa pia kuzisaidia nchi nyingi iwezekanvyo za Afrika.

Amesema lengo ni kutaka kuona kwamba nchi hizo zinaboresha Taknolojia yake kitendo kitakachopunguza matatizo ya Nishati ya Umeme.

Naye Profesa Vladimir Shubin kutoka taasisi ya elimu ya Kiafrika mjini Moscow ameliambia Shirika la habari la IPS kwamba ziara ya rais Mubarak imeamsha maenedeleo zaidi ya ushirikiano baina ya Russia na Misri na pia baina ya Viongozi wa nchi hizo mbili.

makubaliano hayo pia yameihakikishia Russia kuwa na ushirikiano zaidi wa pande hizo mbili kwa njia ya matumizi ya nishati ya Kinyuklia kwa malengo ya amani.

Akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na Rais Mubarak wa Misri, Rais wa Russia Vladimir Putin alisema mpango huo umeweza kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya nchi hizo.

Rais Putin amesema Misri ni mshirika mkubwa wa Russiana kwamba ushirikiano wao upo katika masuala ya kisiasa na kiuchumi na wanatazamia baadaye kuuendeleza zaidi katika juhudi za kuimarisha masuala ya Kiuchumi.