Rwanda yakanusha kukiunga mkono kikundi cha waasi cha M23
16 Julai 2012Matangazo
Mwishoni mwa juma wapiganaji 24 wa kikundi hicho ambao walidai ni raia wa Rwanda walijisalimisha kwenye jeshi la Umoja wa Mataifa na kuomba warudishwe nyumbani. Lakini mpakani, Rwanda ilikataa kuwapokea wapiganaji hao na kuwarudisha nyuma. Daniel Gakuba amezungumza kwa njia ya simu na waziri wa usalama wa ndani wa Rwanda, Fadhil Harerimana, na kwanza alimuuliza, kwa nini Rwanda iliwakataa wapiganaji hao waliojisalimisha.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Danieli Gakuba
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman