1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda,Jamhuri ya Afrika Kati na Ebola Magazetini

4 Aprili 2014

Miaka 20 tangu mauwaji ya halaiki yalipotokea Rwanda,uamuzi wa umoja wa Ulaya kutuma wanajeshi jamhuri ya Afrika kati na kitisho cha kutapkaa Ebola ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi magazetini wiki hii.

https://p.dw.com/p/1Bbx1
Wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa wakisiammia opereshini Turquoise nchini Rwanda kabla ya mauwaji ya halaiki ya mwaka 1994Picha: P.Guyot/AFP/GettyImages

Tunaanzia na kumbukumbu za miaka 20 ya mauaji ya halaiki yaliyoangamiza maisha ya zaidi ya watutsi laki nane na wahutu wa misimamo ya wastani nchini Rwanda.Wahalifu wanaishi "raha mustarehe" ndio kichwa cha maneno cha gazeti la Frankfurter Allgemeine linalochambua kitabu kilichoandikwa na Jean Hatzfeld anaehisi pengine wahalifu hawana hofu kwasababu Ufaransa imekaa kimya.Jean Hatzfeld ameandika vitabu vitatu kuhusu mauwaji ya halaiki ya Rwanda na kutunukiwa tuzo ya Médicis mwaka 2007.Cha nne kimechapishwa hivi karibuni nchini Ufaransa kwa jina "Englebert des Collines" au "Englebert wa milimani"kinachosimulia kuhusu maisha ya rafiki yake wa muda mrefu wa kitutsi aliyenusurika na mauwaji ya halaiki ya Rwanda.Baada ya kuelezea uhusiano uliokuwepo kati ya Ufaransa na utawala wa zamani wa wahutu na shambulio lililopelekea rais wa zamani Juvenal Habyarimana kuuwawa ,siku hiyo hiyo usiku mpango uliokuwa umeandaliwa muda mrefu ukatekelezwa-linaandika Frankfurter Allgemeine likinukuu kikilichosimuliwa na mwandishi vitabu Jean Hatzfeld.Anaituhumu Ufaransa kuyafumbia macho yaliyotokea.Na anahoji uchunguzi uliofanywa hivi karibuni umeonyesha ndege aliyokuwa akisafiria Habyarimana ilishambuliwa na wahutu waliokuwa pamoja na wafaransa na sio waasi kama ilivyokuwa ikisemekana.Masuala mengi hayakupatiwa majibi na kipeo cha mchango wa Ufaransa nacho pia hakijafafanuliwa.Hata hivyo kutokana na vitabu vyake na utafiti aliofanya kuhusu mauwaji ya halaiki mwandishi vitabu huyo wa kifaransa aliyezaliwa Madagascar amechangia kuwafanya watu wasisahau kamwe yaliyotokea miaka 20 iliyopita nchini Rwanda-linamaliza kuandika Frankfurter Allgemeine.

Hofu zingalipo yaliyotokea yasije yakajiri tena

Gazeti la mjini Berlin-Berliner Zeitung linazungumzia hofu ya watu,yaliyotokea miaka 20 iliyopita yasije yatatokea tena.Gazeti linasema mika 20 baada ya mauwaji ya halaiki Rwanda imegeuka nchi inayopigiwa mfano wa kuigizwa barani Afrika;usafi umeenea kila pembe,ukuaji wa kiuchumi unafikia asili mia nane kwa mwaka,rushwa inapigwa vita kikamilifu,hata hivyo Berliner Zeitung linasema wanyarwanda wamefikia hali hiyo kutokana na utawala wa kimabavu wa rais Kagame.Maandamano ni marufuku-upande wa upinzani unakandamizwa na vyombo vya habari vinavyoikosoa serikali vinawekewa vizuwizi.

Pengo kati ya makabila mawili makuu,yaani watutsi na wahutu ni pana.Berliner Zeitung linazungumzia hofu iliyoko miongoni mwa jamii yaliyotokea miaka 20 iliyopita yasije yakajiri tena.

Umoja wa Ulaya waamua kutuma wanajeshi Jamhuri ya Afrika Kati

Lilikuwa gazeti la mjini Berlin pia,die Tageszeitung lililozngumzia kuhusu azma ya Umoja wa ulaya kutuma wanajeshi katika Jamhuri ya Afrika kati.Azma hiyo ilifafanuliwa pembezoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na wale wa Afrika mjini Brussels.Utayarifu wa kutuma wanajeshi umepata nguvu baada ya Ujerumani ,Uingereza na mataifa kadhaa ya ulaya ya mashariki kuahidi kuchangia wanajeshi ili kusaidiana na wale wa Ufaransa-Sangaris na wa nchi za Afrika wanaounda kikosi cha Misca kurejesha amani katika nchi hiyo ya Afrika kati.Hali katika Jamhuri ya Afrika kati imezidi kuwa mbaya kwa namna ambayo waumini wa dini ya kiislam wameamua kuuhama mji mkuu Bangui ,linamaliza kuandika Die Tageszeitung.

EU Afrika Gipfel Merkel 02.04.2014 Brüssel
Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Afrika mjini BrusselsPicha: Reuters

Ebola yapata nguvu Afrika Magharibi

Na hatimae wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamemulika kitisho cha kuenea homa ya kuambukiza ya Ebola barani Afrika.Gazeti la Berliner Zeitung linazungumzia mvutano uliozuka kati ya shirika la afya la umoja wa mataifa WHO na shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Médécins Sans Frontières kuhusu kipeo halisi cha maradhi hayo ya hatari kabisa ulimwenguni yaliyoenea katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi.Katika wakati ambapo Shirika la WHO linazungumzia juu ya kipeo kinachokadirika,shirika la Madaktari wasiokua na mipaka linaonya maradhi hayo yanaweza kufikia "kipeo kisichokuwa na mfano".Homa ya Ebola inasemekana inaziathiri nchi tatu za Afrika Magharibi:Guinea,Liberia na Siera Leone .Zaidi ya kadhia 120 zimeripotiwa na watu wasiopungua 80 kupoteza maisha yao.Berliner Zeitung linakumbusha homa ya Ebola ilikwisha ripotiwa katika miaka ya 95 karibu na mji wa Kongo wa Kikwit ambako watu 25 walifariki dunia.

WHO Ebola Afrika Schutzanzüge
Madaktari wa shirika la afya la Umoja wa mataifa nchini GuinePicha: Isaac Kasamani/AFP/Getty Images

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/BASIS/PRESSER/ALL/presse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman