1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RYAD: Wapalestina watolewa wito wa kukomesha mapigano kati yao

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6X

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bibi Condoleeza Rice, ameyatolea mwito makundi ya wapalestina kumaliza uhasama na mapigano kati yao. Ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Jeddah nchini Saudi Arabia, hatua ya kwanza ya ziara ndefu katika eneo la mashariki ya kati. Amesema raia wasiyokuwa na hatia wamekuwa wakinasa katika mapigano kati wafuasi wa chama cha Fatah na wale wa chama cha Hamas ambayo yameshapelekea watu 12 kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Bibi Condoleeza Rice sasa amewasili mjini cairo nchini Misri kwa mazungumzo na viongozi wa kiarabu kuhusu mbinu za kuzisaidia serikali za Iraq, Lebanon na Palestina zinazokabiliwa na machafuko.