1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saddam anyongwa

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeq

TAARIFA YA HABARI 30-12-06 16.00

BAGHDAD:

Rais wa zamani wa Iraq,Saddam Hussein, amenyanogwa mapema asubuhi ya leo baada ya adhabu yake ya kifo aliyopitishiwa mwezi uliopita kwa mchango wake katika mauaji ya watu kiasi cha 150 katika mji mdogo wa Dujail wa washiia kuthibitishwa i na Mahkama ya Rufaa.

Sasa inazingatiwa wapi hasa azikwe.Kuna taarifa zinazosema maiti ya Saddam haitakabidhiwa jamaa zake kwa hivi sasa na kwamba ingeezikwa mahala pasiri.

Baada ya kunyongwa Saddam, mripuko mkubwa ulitokea katika soko la samaki huko Kufa, kusini mwa m ji mkuu Baghdad na km 160 kutoka Baghdad.Watu si chini ya 31 wameuwawa na wengine 50 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Na katika wilaya ya Huriya inayokaliwa pia zaidi na washiia,mjini Baghdad, bomu limeua watu 8 na kuwajeruhi wengine 18.

Taarifa kutoka MAHMUDIYA –zinasema maiti za watu 4 walioteswa na kupigwa risasi zimegunduliwa huko ,maili 20 kutoka Baghdad.

Bomu lililotegwa barabarani limemuua askari mmoja wa kimarekani na kuwajeruhi 2 wengine kaskazini-magharibi mwa Baghdad hapo jana.