1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sakata ya mafuta Visiwani Zanzibar

29 Aprili 2009

Katika miezi michache iliopita kumekuweko tetesi na hata mazungumzo hadharani huko Visiwani Zanzibar juu ya visiwa hivyo kuwa na akiba ya mafuta.

https://p.dw.com/p/HgXc
Rais Jakaya Kikwete wa TanzaniaPicha: DW

Hivyo, kukazuka majadiliano makali kama mafuta hayo pindi yakichimbuliwa yasimamiwe na kumilikiwa na serikali ya Muungano wa Tanzania au na ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini jana Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania alisema kwamba hakujagunduliwa mafuta Zanzibar. Ikiwa ni hivyo, jee kulikuweko haja ya mabishano juu ya jambo hilo yaliozagaa hapo kabla huko Zanzibar?

Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman

Othman Miraji alimpigia simu waziri wa nishati wa serikali ya Zanzibar, Mansur Yusuf Himid, ili kupata ufafanuzi zaidi...