1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Salih Osman kutunukiwa tunzo ya Sacharow

11 Desemba 2007

Mwanaharakati mpigania haki za binaadamu kutoka Sudan Salih Osman, leo anatunukiwa tunzo ya Sacharow na bunge la ulaya mjini Strassburg .

https://p.dw.com/p/Ca5z
Salih Mahmoud Osman
Salih Mahmoud OsmanPicha: presse

Osman ambaye ni mwanasheria aliwahi kuwekwa korokoroni na watawala wa nchi hiyo kwa muda wa miezi saba.

Wapigania haki za binaadamu kutoka Zimbabwe na Sudan walitoa wito Jumanne leo mjini Brussels kuutaka umoja wa ulaya utowe shinikizo zaidi kwa watawala wa nchi hizo mbili juu ya kulindwa na kuheshimiawa haki za binaadamu.

Mshindi wa tunzo ya Sacharow, Salih Osman ambaye atapokea tunzo hiyo hii leo, anasema hali akatika jimbo la Darfur inazidi kuwa mbaya. Viji vinapigwa mabomu na kunafanyika visa vya kila aina vya matumizi ya nguvu, huku utawala nchini mwake ukiendelea kuepuaka hali yoyote ya mapatano na jumuiya ya kimataifa kuhusu njia za kuutatua mgogoro huo.

Osman binafsi aliwekwa ndani kwa miezi saba na aliachiwa huru tu baada ya kuanza mgomo wa kula chakula . Jamaa zake waliteswa na nyumba zao kuchomwa moto na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali. Tunzo ya Sacharow ya bunge la ulaya , imepewa jina la mwanafizikia Andrei Sacharow ambaye wakati wa uhai wake alisimama kidete kuukosaoa utawala wa iliokua Urusi ya zamani akipinga kukandamizwa kwa haki za binaadamu nchini humo.

Kwa upande wake Osman amekua takriban kwa miaka 20 sasa akiwatetea wahanga wa ukandamizaji wa haki za binaadamu. Akizungumzia kutunukiwa kwake tunzo hiyo anasema ,“Tunzo ya Sacharow ni ishara kwetu sote wapigania haki za binadamu kwamba mchango wetu unatambuliwa na bunge la ulaya na sote tunashuku kupokea tunzo hii kwa niaba ya mamia ya wanaopigania haki za binaadamun katika Darfur na Sudan kwa jumla, wanaoamini juu ya haja ya kutafuta haki.“

Miongoni mwa juhudi za Bw Osman ni kuwasaka wanaohusika na ukiukaji wa haki za binaadamu katika Darfur na kuwaorodhesha ili wafikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa mjini The Hague. Lakini pamoja na hayo amelalamika juu ya ukosefu wa hataua za kivitendo kwa upande wa jamii ya kimataifa, akisema ,“Tuna zaidi ya maazimio 15 ya umoja wa mataifa kuhusu Darfur, lakini hata moja halijatekelezwa . Ni maneno matupu tu karatasini."

Mwanaharakti huyo mpigania haki za binaadamu Dafur , akaongeza kwamba wanachokihitaji ni kila msaada unaowezekana ili kuzuwia maafa ya wakaazi wa Darfur.

Bw Osman akasema kwamba kwa upande wa Umoja wa ulaya , hadi sasa haujawa na msimamo thabiti, akisisitiza kwamba hauhitaji tena kujadiliana iwapo kinachotokea Darfur ni mauaji ya kimbari au la, wakati ambapo maelfu wameuwawa na wanazidi kuuwawa.

Akakumbusha kwamba mtu hana haja ya kujifunza mengi wakati ambapo wakati ambapo takriban watu milioni 3 wamelazimika kukimbilia nchi jirani kujinusuru.

Tunzo ya Sacharow kwa ajili aya haki za binaadamu inatolewa na bunge la ulaya tangu 1998 na inaambatana na kitita cha fedha cha Euro 50,000 .

Washindi waliotangulia wa tunzo hiyo ni pamoja na Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson mandela na kiongozi wa upinzani nchini Belaruss Alexander Milinkewitsch.