1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAMARRA:Mashambulio ya kimadhehebu yaongezeka Iraq

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs3

Wapiganaji wameripua minara miwili ya msikiti muhimu wa madhehebu ya washia ulioko kwenye mji wa kaskazini wa Sammarra.

Shambulio hilo la bomu dhidi ya msikiti wa Al Askari unaojulikana pia kama mkiti wa dhahabu lilitekelezwa licha ya kuwepo vikosi vya usalama kwenye eneo hilo.

Msikiti huo umewahi kushambuliwa mwaka jana mnamo mwezi wa Februari na kuzusha wimbi la mauaji ya kimadhahebu kote nchini humo.

Wakati huo huo misikiti minne ya wasunni imeshambulio leo hii na kuonekana kama ni hatua ya kulipiza kisasi iliyofanywa na washia.

Misikiti mitatu imeshambuliwa katika mji wa Iskandiriyah na mmoja katika eneo la Bayaa karibu na mji wa Baghdad.

Serikali ya Iraq imesema imetangaza hali ya watu kutotoka nje kwa muda usiojulikana katika mji mkuu Baghdad ili kuzuia ghasia zaidi kutokea.