1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANA’A : Wakimbizi wa Somalia wafia baharini

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfM

Mashua mbili zilizokuwa zimebeba watu waliokuwa wakikimbia kutoka Somali zimepinduka nje ya mwambao wa Yemen na kuuwa watu 17 na wengine 140 hawajulikani walipo.

Wengi wa wakimbizi hao wanasema wanakimbia mapigano yaliozuka hivi karibuni kusini mwa Somalia na katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema mojawapo ya mashua hiyo ilipinduka baada ya abiria wake kufadhaika kutokana na kugunduliwa na mashua za polisi za Yemen.Mashua ya pili ilizama wakati ilipokuwa ikirudishwa ufukweni na mashua za walinzi wa mwambao wa Yemen pamoja na helikopta.

Kwa mujibu wa UNHCR mashua hizo mbili zilizozama zilkuwa miongoni mwa mashua nne zilizokuwa zikiwasafirisha kwa magendo abiria 515.

Abiria wengine 317 walionusurika walipelekwa kwenye kituo cha wakimbizi cha UNHCR kilioko Myfaa kusini mashariki mwa jimbo la Shabwa kama kilomita 460 kutoka mji wa Sana’a.