1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA:Wahispania saba wauawa katika shambulizi la kigaidi

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmF

Watalii saba wa Uhispania na raia wawili wa Yemen wameuawa katika shambulizi la kigaidi la kujitoa mhanga huko Yemen.

Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania imesema kuwa watu wengine wawili walijeruhiwa katika shambulizi.

Wizara ya mambo ya ndani ya Yemen imewalaumu wanachama wa kundi la Al Qaida kwa kuhusika na shambulizi hilo lililotokea katika mji wa Marib kiasi cha kilomita 150 kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen Sanaa.