1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO : Bachelet hatohudhuria maziko ya Pinochet

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCk9

Dikteta wa zamani wa Chile Augusto Pinochet atazikwa hii leo kwa heshima za kijeshi.Hapo awali,rais Michelle Bachelet wa Chile alisema, kiongozi huyo wa zamani hatopewa maziko ya heshima rasmi na wala hakutokuwepo siku rasmi ya msiba.Wakati wa utawala wa Pinochet kiasi ya watu 28,000 walikamatwa na kuteswa na mamia elfu ya Wachile walikimbilia nchi za ngámbo.Waziri Mkuu Bachelet,akiwa miongoni mwa Wachile waliokuwa uhamishoni wakati wa utawala wa kidikteta wa Pinochet,hatohudhuria mazishi ya leo.