1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO : Moto wauwa wafungwa 29 gerezani

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79i

Moto ambao uliwashwa kwa makusudi kwenye gereza kaskazini mwa Argentina umeuwa takriban wafungwa 29.

Moto huo uliwaka kwenye gereza hilo baada ya wafungwa wanaopinga mazingira ya mahabusu kuyatia moto magodoro yao.

Gereza hilo la mkoa lina wafungwa wapatao 500.