1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Santiago . Mwakilishi wa serikali azomewa katika mazishi ya Pinochet.

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjn

Nchini Chile , waombolezaji katika mazishi ya dikteta wa zamani Augusto Pinochet , wamemzomea mwakilishi pekee wa serikali katika mazishi hayo.

Waziri wa ulinzi Vivianne Blanlot, alizomewa kwasababu serikali imekataa kumpa Pinochet mazishi ya kitaifa.

Kabla ya mazishi hayo katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Santiago, karibu watu 60,000 walitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza la Pinochet .

Maafisa wanajitayarisha iwapo kutatokea ghasia kati ya wanaomuunga mkono Pinochet na wale wanaompinga. Siku ya Jumatatu waandamanaji tisa walikamatwa baada ya mapambano na polisi.