1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO : Pinochet azikwa kwa heshima za kijeshi

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCju

Mazishi ya heshima za kijeshi ya dikteta wa zamani wa Chile Augusta Pinochet yamekuwa yakiendelea kufanyika mjini Santiago na kuhudhuriwa na jamaa zake kadhaa, marafiki na maafisa waandamizi wa jeshi la Chile.

Tokea kifo chake hapo Jumapili wapinzani wa kiongozi huyo wa zamani wameingia mitaani mjini Santiago na katika miji mengine kulaani kumbukumbu anayoiwachilia nchi hiyo.

Zaidi ya watu 3,000 waliuwawa wengine 28,000 waliteswa na mamia kwa maelfu wengine waliikimbia nchi hiyo kwenda kuishi uhamishoni wakati wa utawala wa miaka 17 wa Pinochet.

Serikali imemnyima kiongozi huyo mazishi kamili ya kitaifa.