1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAOLO: Papa Benedikt aonya kuhusu maafa ya kijamii

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3M

Papa Benedikt wa 16 akiendelea na ziara yake ya siku tano nchini Brazil aliwahotubia vijana katika uwanja wa mpira mjini Sao Paolo.Kiongozi huyo wa Kanisa la Katoliki aliwaonya vijana dhidi ya madawa ya kulevya,ulajirushwa,uteketezaji wa misitu ya Amazon na uhusiano wa kijinsia kabla ya ndoa.Hapo awali,Papa Benedikt alikutana na Rais Luiz Inacio Lula da Silva mjini Sao Paolo.Kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Brazil,mada mbali mbali zilijadiliwa na viongozi hao wawili, ikiwa ni pamoja na masuala ya elimu na njia za kuimarisha dhima za familia katika jamii.Lakini hawakugusia suala gumu linalohusika na kitendo cha kutoa mimba.Leo hii,Papa Benedikt atasoma misa kwenye uwanja mmoja wa ndege mjini Sao Paolo,ambako atatangaza utakatifu wa mtawa Antonio Galvao wa karne ya 18.