1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAOLO: Pendekezo kufunga uwanja wa ndege wa ajali

19 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBh6

Waendesha mashtaka nchini Brazil wanafikiria kukifunga kiwanja cha ndege cha Congonhas mjini Sao Paolo,wakati uchunguzi ukifanywa kuhusu ajali ya ndege iliyotokea siku ya Jumatano.Katika ajali hiyo,hadi watu 189 walipoteza maisha yao baada ya ndege kushindwa kusimama wakati wa kutua katika hali mbaya ya hewa.Ndege hiyo iligonga kuzuizi na ikaingia barabarani na ikaishia kusimama kwenye jengo la kuhifadhi mizigo na depo ya mafuta na ikaripuka.