1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAULO : Rais Bush aanza ziara Amerika Kusini

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL1

Rais George W. Bush wa Marekani amewasili katika mji mkuu wa fedha na viwanda nchini Brazil hapo jana kuanza ziara ya siku tano ya mataifa ya Amerika ya Kusini yenye lengo la kuimarisha demokrasia na biashara huru.

Masaa machache kabla kuwasili kwa rais huyo mjini Sao Paulo polisi ilifyetuwa mabomu ya kutowa machozi baada ya zaidi ya watu 6,000 kuandamana katika maandamano ya amani pia imeripotiwa kwamba wafuasi wa kundi la sera za mrengo wa shoto wanaofikia 200 wamevurumisha mawe kwenye ubalozi mdogo wa Marekani ulioko mjini humo.

Bush ambaye amekuwa akikosolewa kwa kuipuza Amerika ya Kusini ameahidi wiki hii kuunga mkono haki katika jamii na kukuza uchumi wa eneo hilo na kuzinduwa miradi ya misaada kwa ajili ya elimu,nyumba na afya.

Mapambano kati ya polisi na waandamanaji wanaopinga ziara ya Bush pia yameripotiwa kutokea nchini Colombia ambapo Bush anatarajiwa kuzuru hapo kesho na huko Guatemala kundi la watu wa makabila asilia la Wamayan limesema litatakasa maeneo atakayotembelea Bush baada ya ziara yake kwa kuwa anakwenda huko na pepo wabaya.

Wanamshutumu kwa kuwakandamiza ndugu zao wahamiaji walioko Marekani na kwa vita alivyovianzisha.