1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAULO: Siku tatu za maombolezo nchini Brazil

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhK

Rais wa Brazil Lula da Silva ametangaza siku tatu za maombolezo ya taifa kufuatia ajali ya ndege iliyotokea kwenye uwanja wa ndege wa Congonhas. Rais Horst Köhler wa Ujerumani pia ametoa salamu za rambirambi kwa jamaa waliokumbwa na msiba huo.Kiasi ya watu 200 wamepoteza maisha yao baada ya ndege ya shirika la TAM la Brazil kutereza kwenye njia ya kutua.Ndege hiyo aiana ya Airbus A320,iligonga kizuizi cha uwanja wa ndege na kuingia barabara kuu kabla ya kusimama katika kituo cha petroli na kushika moto.Inadhaniwa kuwa hali mbaya ya hewa ndio imesababisha ajali hiyo. Shirika la Airbus la Ulaya linalotengeneza ndege, limepeleka Brazil wataalamu wake watano kusaidia kuchunguza kile kilichosababisha ajali hiyo.