1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAULO:Ndege ya Tam yadondoka uwanja wa ndege wa Conganhas

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBha

Ndege ya Shirika la ndege la Tam nchini Brazil imedondoka baada ya kuteleza kwenye barabara iliyo na maji kwenye kiwanja cha ndege cha Congonhas.Abiria 170 pamoja na wahudumu 6 walikuwa safarini katika ndege hiyo iliyogonga jengo moja na kushika moto.Watu wanane wanaripotiwa kujeruhiwa na mmoja kufariki katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ilitua kutoka eneo la Porto Alegre lililo kusini na kuteleza kwenye barabara ya ndege iliyokuwa na maji kwasababu ya mvua.Watu wanane ambao ni wafanyikazi wa shirika hilo waliokuwamo ndani ya jengo lililogongwa na ndege hiyo walijeruhiwa kwas mujibu wa kituo cha televisheni cha Globo.

Kulingana na kampuni ya ndege ya Tam malori 31 ya kuzima moto yako katika eneo hilo ili kupambana na moto uliotokea baada ya ndege kudondoka.Uwanja wa ndege wa Congonhas ulio mjini umefungwa pamoja na barabara zote zinazoelekea huko.