1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SARAJEVO: Rais wa Ujerumani akamilisha ziara yake

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBld

Rais wa Shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler anamaliza ziara yake katika nchi za Balkan hii leo kwa kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani wanaotumikia kikosi cha Umoja wa ulaya cha kulinda amani nchini Bosnia-Herzegovina.

Wanajeshi hao wa Umoja wa Ulaya wamepewa jukumu la kusimamia makubaliano ya amani ya Dayton yaliyomaliza vita vya Bosnia vya miaka 12 iliyopita.

Awali rais wa Shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler alizitembelea pia Romania na Bulgaria na kuzungumza na viongozi wa nchi hizo.