1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarkozy kuzungumza na Brown leo.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVf0

London.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anapanga kuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown tena katika siku ya pili na mwisho ya ziara yake nchini Uingereza.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wawili wanatarajiwa kukamilisha makubaliano kuhusiana na vinu vipya vya nishati ambavyo vitasaidia kuzuwia ongezeko la ujoto duniani.

Jana Jumatano , Sarkozy amesema kuwa mataifa hayo mawili yamekuwa yakiunga mkono kwa nguvu zote manufaa ya nishati ya kinuklia.

Tamko linalolenga kupambana na uhamiaji haramu pia linatarajiwa.

Katika hotuba yake kwa mabunge yote nchini Uingereza , jana , Sarkozy amesema kuwa Ufaransa na Uingereza hazijakaribiana kuliko ilivyo hivi sasa na kwamba Ulaya inaihitaji Uingereza.

Na akaongeza kuwa atapendekeza kuongeza majeshi ya nchi yake nchini Afghanistan katika mkutano wa NATO mjini Bucharest wiki ijayo.

Ziara hiyo ya siku mbili ni ya kwanza rasmi kwa rais wa Ufaransa nchini Uingereza katika muda wa miaka 12.