1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarkozy -Moscow

9 Septemba 2008

Rais wa Ufaransa Sarkozy apata ridhaa ya Urusi kuondoa majeshi Georgia.

https://p.dw.com/p/FE9E
Sarkozy na SaarkaschvilliPicha: AP

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa, amemtishia rais Dimitri Medwedew wa Urusi kuwa Umoja wa Ulaya utaiwekea vikwazo endapo haitatimiza ahadi ilizotoa kuondoa majeshi yake kutoka ardhi ya Georgia.

Tarehe ya mwisho iliopewa Urusi kufanya hivyo ni Oktoba 15-hii ni kwa muujibu alivyoarifu Rais Sarkozy wa kufuatia mazungumzo yake na Rais Michail Saarkaschwili wa Georgia jana usiku mjini Tiflis.

Hapo kabla, rais Sarkozy alifaulu kupata ridhaa ya Moscow kuondoa majeshi yake kutoka Georgia mnamo muda wa mwezi mmoja na kuyarudisha pale yalipokuwapo kabla vita kuripuka mwanzoni mwa August.

Je, rais wa Umoja wa Ulaya, Sarkozy amepasi mtihani wake na sasa anaweza kuvuta pumzi ? Urusi imeregeza kamba na imeridhia sasa kuondoa majeshi yake mnamo muda wa mwezi kutoka Georgia.Urusi ilikwisha mara moja kuridhia kufanya hivyo pale ilipoafikiana na Sarkozy wiki 4 hivi zilizopita mpango wa mambo 6.Sasa ni mwezi ujao wa Oktoba utakodhihirisha dhahiri-shahiri kwa kadiri gani yafaa kuiamini Moscow.

Kwani hivi sasa ni kusubiri kutimiza rais Medwedew ahadi aliotoa.

Kwa kuridhia pia Medwedw Tume ya wachunguzi ya Umoja wa Ulaya

iende Georgia,yafaa kutegemea itaruhusiwa kufanya hivyo.Yafaa lakini mtu kuweka shaka shaka zaidi upande wa sehemu ya pili ya maafikiano yao.Kuhusu hadhi za maeneo ya Ossetia ya kusini na Abkhazia,ingawa Moscow itayari kulizungumzia swali hilo katika daraja ya kimataifa,mtu asiitazamie kufuta hatua yake ya kuyatambua maeneo hayo kama ni nchi huru.

Umoja wa Ulaya unapaswa kwahivyo kumeza kidonge hicho kichungu.

Muhimu zaidi ni kuwa Urusi inahamisha majeshi yake kutoka ardhi ya Georgia na hii kwa manufaa ya Georgia na ya umoja wa Ulaya.Ingelikua balaa kubwa laiti Sarkozy na uongozi wa UU ungerudi kutoka Moscow mikono mitupu......

Miongoni mwa wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya kuna waliotaka kuchukuliwa Urusi hatua kali na laiti pasigefikiwa muwafaka,basi pengine ufa ndani ya Umoja wa Ulaya unegelikua hata mkubwa zaidi.

Na hii ilitambua Moscow.Kwani, kwa Urusi Umoja wa Ulaya kama ngome ya kiuchumi ni mshirika anaefaa sana kimkakati.Kwani sio tu Urusi inataka kuuzia nishati yake ilio ghali bali inahitaji hata fedha zake kwa kuiuzia gesi yake.Kwa jicho hili ,haikuwa kwa manufaa ya Urusi kupalilia mpasuko zaidi ndani ya Umoja wa ulaya.

Rais mpya wa Urusi aliwapa baadhi ya wachambuzi wa maoni sababu ya kuhisi vita baridi vimefufuka .....

Urusi imecheza karata zake kwa nguvu mno na imepoteza kiasi fulani ushawishi wake.Kujiingiza kijeshi Georgia na kutambuliwa na nchi za Umoja wa Ulaya Kosovo kama nchi huru, kulitumiwa na Moscow kama chambo kuwabainisha tangu wananchi nchini Urusi hata na hata ngambo kuwa Ulaya itajikuta inachachatika kwa baridi endapo ikimchokoza Bweha wa Urusi.Hapo Russia imetimiza shabaha yake muhimu.

Kumesalia swali moja :Urusi itaendelea kubisha hodi hodi za Ukraine na Georgia kujiunga na shirika la