1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarrazin akosolewa vikali

30 Agosti 2010

Thilo Sarrazin,mwanachama wa Bodi ya Benki Kuu ya Ujerumani, amekosolewa vikali na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle na Baraza Kuu la Wayahudi kuwa anachochea ubaguzi na chuki dhidi ya Uyahudi.

https://p.dw.com/p/OzDM
Thilo Sarrazin nimmt am 15. Oktober 2009 an einer Podiumsdiskussion zum Thema "Ordnungspolitische Rahmenbedingungen der Finanzmaerkte" in Berlin teil. Ungeachtet der heftigen Kritik an seinen vielfach als auslaenderfeindlich empfundenen Aeusserungen hat Bundesbank-Vorstandsmitglied Thilo Sarrazin am Samstag, 28. August 2010, nachgelegt. Der "Welt am Sonntag" sagte er, muslimische Migranten integrierten sich ueberall in Europa schlechter als andere Einwanderergruppen. (AP Photo/Franka Bruns) --- FILE - Former Finance Senator of Berlin, Thilo Sarrazin, participates in a discussion in Berlin, Oct. 15, 2009. (AP Photo/Franka Bruns)
Mwanachama wa Bodi ya Benki Kuu ya Ujerumani, Thilo Sarrazin.Picha: AP

Chama cha SPD hakimtaki tena kama mwanachama na viongozi wa SPD wametoa mwito kwa Sarrazin kuondoka chamani. Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema haiwezekani kabisa kuyakubali matamshi ya Sarrazin.

Kufuatia matamshi ya utata ya Thilo Sarrazin kuhusu wahamiaji wa Kiislamu nchini Ujerumani yaliyokosolewa vikali, sasa mwanachama huyo wa Bodi ya Benki Kuu ya Ujerumani "Bundesbank" na chama cha SPD, amekosolewa upya kwa maoni yake kuwa Wayahudi wana jeni ya aina moja.Vile vile amesema, wahamiaji wa Kiislamu barani Ulaya hawataki au hawawezi kujijumuisha katika jamii za nchi za magharibi.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) gestikuliert am Montag, 23. August 2010, vor der Sitzung des CDU-Vorstands in Berlin. (apn Photo/Berthold Stadler)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hayo ni matamshi yasiokubalika hata kidogo. Matamshi hayo yanavuka mpaka na yanaonyesha chuki dhidi ya makundi fulani katika jamii. Ubaya zaidi, Sarrazin anadai kuwa anashughulikia mada hiyo, lakini matamshi yake hayasaidii hata kidogo. Amesema:

"Suala la kuwajumuisha wahamiaji ni mada iliyo muhimu sana katika jamii yetu. Nimewaalika ofisini kwangu wajumbe wanaoshughulikia mada hiyo na tumefanya kazi kubwa - na bado kuna kazi nyingi za kufanywa. Lakini vile anavyozungumza, atasababisha mgawanyiko katika jamii na hiyo itakwamisha majadiliano."

Wakati huo huo, Naibu Kansela na Waziri wa Mambo ya Nje,Guido Westerwelle, amesema matamshi ya kuchochea ubaguzi au chuki dhidi ya Uyahudi hayana nafasi yo yote ile katika majadiliano ya kisiasa. Nae waziri wa ulinzi, Karl-Theodor zu Guttenberg, ameuliza iwapo Sarrazin anafaa kubakia katika Bodi ya Benki Kuu. Amesema, hata uchokozi una mipaka na ni dhahiri kabisa kuwa Sarrazin ameivuka mipaka hiyo kwa matamshi yake yasiofaa.

Kilichozusha hasira ni matamshi mapya ya Sarrazin kuwa watu wenye asili mbali mbali wana jeni tofauti. Akawataja Wayahudi na Wabasque. Baraza Kuu la Wayahudi limesema, matamashi hayo ni chuki ya kibaguzi. Sasa hata katika chama cha SPD, sauti zinazidi kupazwa kupinga uanachama wa Sarrazin. Kiongozi wa SPD katika jimbo la Berlin, Michael Müller amesema, chama hakiwezi tena kumvumilia mwanachama anaekwenda kinyume na maadili ya chama chake. Viongozi wa ngazi za juu katika chama cha SPD wamemshauri Sarrazin kuondoka kwa hiyari, lakini mwanachama huyo amepinga pendekezo hilo.

Mwandishi: Müller,Andrea/ZPR/P.Martin/RTRE

Mhariri: Miraji Othman