1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sasa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuiwekea vikwazo Syria

26 Novemba 2011

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inajiandaa kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Syria, baada ya serikali ya nchi hiyo kushindwa kusaini makubaliano ambayo yangeliruhusu waangalizi huru kuingia Syria.

https://p.dw.com/p/13Hao
Rais Bashar Assad wa Syria.
Rais Bashar Assad wa Syria.Picha: AP

Tangazo hilo la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limesababisha maandamano mapya nchini Syria. Waandamanaji wanaonesha uungaji mkono wao kwa wanajeshi walioasi, Free Syrian Army, ambao sasa wanadai kufikia 20,000.

Mapema Rais Bashar al-Assad alitoa kauli nzito dhidi ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya Jumuiya hiyo. Shirika la Habari la serikali ya Syria, SANA, limesema kwamba Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, imekuwa nyenzo ya uingiliaji kati wa kigeni, na kwamba inatekeleza ajenda ya nchi za Magharibi ya kuliingiza eneo la Mashariki ya Kati, kwenye matatizo. Umoja wa Mataifa unasema kwamba, machafuko nchini Syria yameshagharimu zaidi ya maisha ya watu 3,500, tangu yalipoanza hapo mwezi Machi.

Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR

Mhariri: Prema Martin