1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saumu MWasimba

10 Februari 2017

Mfahamu Saumu Mwasimba, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.

https://p.dw.com/p/2XKRs
DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Picha: DW/L. Richardson

1.    Nchi ninayotokea: Japo shina lang uni Tanga Tanzania,nimezaliwa na kusomea Mombasa na Nairobi Kenya

2.    Mwaka nilipojiunga na DW: Nimejiunga na DW Kiswahili miaka 12 iliyopita

3.    Nilivyojiunga na DW: Nilijiunga DW nikiwa nimeshapata ujuzi kutoka vituo mbali mbali vya Redio na Televisheni nchini Kenya.Nilipata nafasi ya kujiunga Dw nikitokea hasa Royal Media Kenya nikifanya kazi na Redio Citizen na Citizen TV 

4.    Kwanini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Uandishi habari kwangu ni mwito wa kuwatumikia raia wenye kiu ya kuujua ulimwengu na hususan hali halisi katika nchi zao. Kwasababu hii kuu nilijiamini tangu nikiwa msichana mdogo kwamba ninayo sauti na uwezo wa kuyachanganua mambo na kuyafuatilia na hatimae kutowa habari sahihi kwa wananchi.

5.    Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Kwa ninavyoamini mimi kwanza unalazimika uwe na jicho la habari na uelewa mpana katika nyanja mbali mbali. Hiki kwangu nikgezo nambari moja kabla ya vingine vingi.Lakini pia kikubwa bila ya kujiamini katika unachokisimamia siwezi kuamini utasimama katika uandishi habari.

6.    Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Ni mengi yanayoweza kukatisha tamaa katika kazi hii ila nimejifunza kupambana na kuwa mpambanaji wa kweli tena wakujiamini. Sio lele mama kuwa mwandishi wa kimataifa,naweza kuorodhesha changamoto na ukurasa usitoshe kwahivyo wacha niseme, changamoto hazikosekani muhimu ni kwamba kila mara nimekuwa nikijifunza kupitia changamoto hizo badala ya kukata tamaa.

7.    Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Hakika kwangu mimi binafsi nisema kuja kuanza maisha Ulaya tena Peke yangu bila wazazi ni tukio la kihistoria ambalo sitolisahau na mitihani yake.

8.    Mtu ambaye ningependa kumhoji: Kwa miaka 12 niliyoitumikia DW Kiswahili nimewahoji watu mbali mbali viongozi na hata waasi na raia wa kawaida lakini ningependa sana kumhoji rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf niuelewe ukakamavu wake katika uongozi wa nchi iliyoshuhudia miaka kadhaa ya vita, aliyoweza kuifikisha ilipo sasa Liberia.