1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schäuble aagwa na mawaziri wa Euro

Oumilkheir Hamidou
10 Oktoba 2017

Wolfgang Schäuble amekuwa miongoni mwa waliokuwa na usemi wa mwisho katika vikao vya mawaziri wa fedha wa umoja wa Ulaya, katika kikao chake cha mwisho, mawaziri wenzake wa Umoja wa Ulaya walimpa heshma zinazomtahiki.

https://p.dw.com/p/2lYii
Luxemburg Finanzministertreffen Wolfgang Schäuble
Picha: Reuters/E. Vidal

Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya wametaka kumpa hishma zote zinazomstahiki waziri wa fedha anaemaliza mhula wake katika serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble, alipohudhuria kikao cha mwisho cha baraza la mawaziri wa fedha wa Umoja wa ulaya. Idadi kubwa ya mawaziri wameitumia fursa hiyo kumshukuru kwa michango, fikra na bidii zake" amesema mkuu wa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro Jeroen Dijsselbloem  mjini Luxemburg."Daima alikuwa akitanguliza mbele masilahi ya muda mrefu na utulivu wa kanda ya euro" amesisitiza.

Wolfgang Schäuble anatazamiwa kuchaguliwa kuwa spika mpya wa bunge la shirikisho la jamhuri ya Ujerumani-Bundestag, Oktober 24 mwezi huu. Kwa kulitumikia kwa muda wa miaka 8 baraza la mawaziri wa fedha wa umoja wa ulaya, Wolfgang Schäuble alikuwa waziri aliyekuwa na umri mkubwa zaidi ya wenzake 19.  Alichangia kwa sehemu kubwa kutoa mwongozo wa nini cha kufanya katika majadiliano kuhusu mzozo uliozikumba baadhi ya nchi za kanda ya Euro. Na hasa Ugiriki-.

Waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble akihudhuria mkutano wa kanda ya Euro mjini Tallinn, Estonia
Waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble akihudhuria mkutano wa kanda ya Euro mjini Tallinn, EstoniaPicha: DW/B. Riegert

Wolfgang Schäuble: Waziri asiyekuwa na mfano

Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire anasema tunanukuu:"Ameshikilia nafasi muhimu katika kuiendeleza jumuia ya Ulaya. Waziri mwenzake wa Italia Pier Carlo Padoan anasema tunanukuu"Alikuwa waziri wa fedha wa aina pekee."

Katika sherehe hizo za kumwaga mwenzao, mawaziri wa fedha wa umoja wa ulaya wamemtunukia Wolfgang Schäuble bendera ya Umoja wa Ulaya na sampuli ya  noti ya Euro 100 yenye picha yake.

Katika mkutano huo Wolfgang Schäuble amesema "tumefanikiwa katika kipindi kigumu. Kanda ya Euro iko imara, tumefanikiwa katika kipindi cha miaka minane ya mzozo wa Euro, kuhakikisha utulivu wa sarafu ya Euro " amesema na kuitaja Ureno kuwa mfano mzuri wa juhudi za Umoja wa Ulaya za kuhakikisha utulivu wa sarafu ya Euro.

Ramani ya nchi wanachama wa kanda ya Euro
Ramani ya nchi wanachama wa kanda ya Euro

Hatima ya mfumo wa kudhamini utulivu wa sarafu ya Euro ESM

Mbali na kumwaga Wolfgang Schäuble mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya wamezungumzia pia nafasi ya siku za mbele ya mfumo wa kudhamini utulivu wa sarafu ESM. Mfumo huo una umuhimu mkubwa, na sio tu katika kukabiliana na mizozo bali pia kuepusha isitokee" amesema kiongozi wa kundi la nchi zinazotumia sarafi ya Euro, Dijsselbloem.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/AFP

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman