1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schalke yakomewa 1:0 na Leverkusen

Ramadhan Ali26 Februari 2007

Katika changamoto za bundesliga,viongozi wa Ligi-Schalke walilazwa jana nyumbani bao 1:0 na Leverkusen.Chelsea imetwaa kombe la Ligi la FA kwa kuipiga kumbo Arsenal 2:1.

https://p.dw.com/p/CHcZ
Bayer Leverkusen yaichapa Schalke 1:0
Bayer Leverkusen yaichapa Schalke 1:0Picha: AP

Tukianza na Ligi mashuhuri za Ulaya, viongozi wa Bundesliga-schalke jana walikiiona kile kilichomtoa kanga manyoya.Walichapwa bao 1:0 nyumbani na kupunguziwa mwanya wao wa uongozi kileleni kwa pointi 2.dakika 5 kabla ya firimbi ya mwisho kulia, mshambulizi wa Bayer Leverkusen stefan Kiessling aliufumania mlango wa Schalke kwa bao pekee jioni hiyo.Schalke wakitazamia kupanua mwanya wao kileleni hadi pointi 7,lakini wamekosa nafasi hiyo.Hasara waliopata hatahivyo haikuwa kubwa kwavile mahasimu wao Werder Bremen wanowafukuzia Schalke kileleni walipoteza nao pointi 2 kwa kumudu suluhu tu ya mabao 2:2 na Borussia Mönchengladbach.Miwhoni mwa changamoto hiyo na Leverkusen, kocha wa Schalke alisema:

“Nafasi nyingi tulizipata kipindi cha kwanza kwa kutamba mno kwa hujuma katika lango la Leverkusen.Kwa bahati mbaya tukashindwa mpira ulipogeuka kwendea upande wetu,kwani tulijua Leverkusen ni hodari kwa kugeuza mchezo haraka namna hiyo.Tulitaka kwa kila hali kushinda nyumbani na tulikua na nafasi nzuri ya kushinda .Kwa bahati mbaya tumeshindwa na hii yatutia uchungu.”

Washindi pekee katika kklabu za usoni walikuwa mabingwa Bayern Munich walioizaba Wolfsburg mabao 2:1 katika Allianz Arena na sasa wanasimama nafasi ya 4 huku mapambano 11 tu yakisalia kabla msimu kumalizika.

Huko Uingereza ilikua finali ya kombe la Ligi ambalo Chelsea-shukurabni kwa bao maridadi la Muivory Coast-Didier Drogba imetoroka nalo.Chelsea ilizaba jana Arsenal London mabao 2:1.Changamoto hii ilijionea kuumia kwa nahodha wa Uingereza john Terry na ngumi uwanjani kati ya Mnigeria John Obi Mikel na nahodha wa Arsenal siku hiyo Kolo Toure.

Katika La Liga-ligi ya Spain, FC Barcelona imefungua mwanya wa pointi 2 kileleni baada ya kuikumta Athletic bilbao 3-0 katika mpambano Samuel Eto’o wa Kamerun alitamba kwa bao la 3 maridadi la Barcelona. Eto’o hakuchezeshwa mpambano uliopita wa champions League pale Barcelona-mabingwa wa ulaya walipozabwa mabao 2:1 na FC Liverpool ya Uingereza.

Huko Ufaransa,viongozi wa Ligi Olympique Lyon walihitaji bao la dakika za mwisho na mkwaju wa bure wa penalty aliouchapa Sylvain Wiltord kutoka suluhu uwani mabao 3:3 na sochaux hapo jumamosi.

Nchini Itali,Inter milan ilisahau kuvunjika kwake moyo kati ya wiki katika champiopns League ilipomudu sare na Valencia kwa kuizaba Catania mabao 5-2.Inter Milan sasa inaongoza Ligi ya Itali kwa pointi 14.Roma inayofuata nafasi ya pili ilitoroka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Reggina.

Sare ya bao 1:1 kati ya Alkamaar na Ajax Amsterdam iliwaruhusu viongozi wa Ligi PSV eindhoven kufungua mwanya wa pointi 7 kileleni mwa ligi ya Holland.

Rais wa shirikisho la kabumbu la Somali Muhydin Hassan Ali anachunguzwa kwa kutoweka kitita cha dala laki 1 –kilichotolewa na FIFA kugharimia mishahara na malipo ya simu –alisema mjumbe mashuhuri wa somalia.

Abdilghani Said –katibu mkuu wa Shirikisho la dimba la Somalia aliarifu kuwa Bw.Muhiydin Hassan Ali eti alitoa kutokla benki kitita cha dala 100.000 na kuacha dala 600 tu katika akiba ya chama hicho.Katika barua FIFA iliomuandikia Hassan Ali ,ilitaka kujua madhumuni ya kutoa fedha hizo.rais wa shirikisho la dimba la Somali kwahivyo, amesimamishw akazi hapo Februari 17.

Hongo pia imelikumba kabumbu nchini Afrika Kusini-nchi inayoandaa kombe la kwanza la dunia 2010:

Kiasi cha miaka 3 tangu kuanzishwa uchunguzi juu ya rushua inayopita katika kabumbu la afrika kusini,mapatano ya biashara za wachezaji ya chini kwa chini ingali ni sehemu ya dimba la humo nchini-gazeti la Sunday times liliripoti jana.Timu hulipa mamiliini ya rand kila msimu ili kupandishwa daraja ya kwanza ya Ligi ya Afrika kusini au kuepuka kuteremshwa daraja.

Rais wa shirikisho la dimba humo nchini Molefi Oliphant amekanusha kujua chichote juu ya hongo katika dimba humo nchini.

Katika ringi ya mabondia, mbabe wa zamani Lennox Lewis wa uingereza, amekanusha ripoti kwamba anapanga kurejea ringini baada ya kustaafu ili kupambana na mbabe wa sasa muukrain Vitali Klitschko.Lewis ana umri wa miaka 41 wakati huu.