1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikli ya Scheswig-Holstein yavunjika

Abdu Said Mtullya21 Julai 2009

Mawaziri wa SPD wafukuzwa kutoka kwenye serikali ya mseto ya jimbo la Schleswig-Holstein.-

https://p.dw.com/p/IudA
Waziri Mkuu wa jimbo la Schleswig-Holstein Peter Harry CarstensenPicha: AP



Serikali ya mseto ya jimbo la Schleswig- Holstein, kaskazini mwa Ujerumani, imevunjika, na waziri mkuu amewafukuza kazi mawaziri wanne.

Waziri Mkuu wa jimbo hilo la Schleswig-Holstein, bwana Peter Harry Carstensen wa chama cha CDU, amewafukuza mawaziri wanne wa chama cha SPD ili kutayarisha kura ya imani bungeni alhamisi ijayo kwa lengo la kuivunja rasmi serikali.Waziri mkuu huyo amechukua hatua baada ya kushindwa kulivunja bunge.

Waziri mkuu Carstensen amesema uamuzi wa kuwafukuza kazi washirika hao wa serikali yake haukuwa rahisi.Serikali ya mseto ya jimbo la Schleswig Holstein, kaskazini mwa Ujerumani iliundwa kutokana na vyama vya CDU na SDP.

Hapo awali, wajumbe wa chama cha SPD walipiga kura kumpinga waziri mkuu Carstensen bungeni alipojaribu kuwasilisha hoja ya kulivunja bunge ili kuitisha uchaguzi.Waziri mkuu huyo hakufanikiwa katika shabaha hiyo kwa sababu chama chake hakikuweza kupata theluthi mbili za kura. Waziri Mkuu Carstensen sasa anakusudia kuitisha kura ya kutokuwa na imani alhamisi ijayo.Lakini wabunge wa SPD na wa vyama vya upinzani wamesimama imara kumpinga. Hatua hiyo itakuwa na maana ya kuvunjika kwa serikali ya waziri mkuu Carstensen.

Chama cha waziri Mkuu huyo ,CDU kinaongoza katika kura za maoni pia katika ngazi ya kitaifa.Mwenyekiti wa chama hicho katika ngazi ya kitaifa, Kansela Angela Merkel, anatarajiwa kushinda katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani utakaofanyika tarehe 27 mwezi septemba. Waziri mkuu wa jimbo la Schleswig-Holstein anakusudia kuitisha uchaguzi wa jimbo lake pia katika siku hiyo ya uchaguzi mkuu.

Mwandishi/Mtullya.A

Mhariri: Miraji Othman