1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asema Ujerumani haitaitupa mkono Sahel

12 Aprili 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema anataka nchi yake iendelee kuwa jukumu kwenye mataifa ya Sahel ambayo yanatawaliwa na majenerali baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4ehA8
Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Andreas Solaro/AFP/Getty Images

Akihutubia halfa ya kutambua mchango wa kikosi cha jeshi la Ujerumani kilichokuwa nchini Mali, Scholz amesema kamwe hawataitupa mkono kanda ya Sahel kwa sababu yoyote. 

Kwa maoni ya kiongozi huyo, kitisho cha kigaidi kutoka kwenye kanda hiyo kinafanya iwe muhimu kuendelea kuisadia Mali kurejesha udhibiti pamoja na kuimarisha usalama kwenye mataifa mengine jirani. 

Kansela Scholz amesema hilo linajumuisha kufanya mazunguzo na watawala wa mataifa ya kanda hiyo hata ikiwa dhahiri kwamva kwamba mashauriano ya aina hiyo yatakuwa magumu. 

Utawala wa kijeshi Mali wazuia shughuli zote za vyama vya siasa

Mali na jirani zake Burkina Faso na Niger zinaongozwa na jeshi baada ya mapinduzi yaliyofanywa miaka ya karibuni na nchi hizo zimeongeza uhusiano wake wa kijeshi na usalama na Urusi. Usuhuba huo ulikilazimisha kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MINUSMA, kuondoka nchini Mali mwishoni mwa mwaka jana. 

Kikosi hicho kilijumuisha wanajeshi kutoka Ujerumani ambao kwa jumla walifikia 20,000 katika kipindi cha miaka 10. 

Hapo jana Scholz aliwashukuru wanajeshi hao katika halfa mjini Berlin na kuahidi kuwa jeshi la Ujerumani Bundeswehr litaendelea kuwa sehemu ya juhudi za kulinda amani duniani.