1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SCHWERIN:Ujerumani mashariki ni muhimu kwa serikali

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKR

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ametangaza kuwa serikali ya Ujerumani inaipa kipa umbele eneo la Mashariki ya Ujerumani linalokabiliwa na uhaba mkubwa wa nafasi za kazi na uwekezaji duni.Bi Merkel aliyasema hayo katika kumbukumbu ya 17 ya muungano wa Ujerumani mashariki na magharibi.

Sherehe hizo zinazoadhimishwa kila mwaka zilitilia mkazo jimbo la Mecklemburg-Pomerania linaloathirika zaidi na matatizo ya kiuchumi na uhamaji.Idadi ya wakazi wa eneo la Ujerumani Mashariki ya zamani imepungua kwa milioni 1.3 kwasababu ya kutafuta maisha bora katika maeneo mengine ya Ujerumani.Eneo la mashariki limebaki nyuma kiuchumi hata baada ya upande wa magharibi kuchangia dola trilioni 3 huku mishahara ikiwa na kima cha chini kwa asilimia 25 na nafasi za kazi kupungua ikilinganishwa na magharibi.

Bi Angela Merkel alizaliwa katika eneo la mashariki ya Ujerumani.