1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scientology kupigwa marufuku ?

9 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CZPr

LISBON:

Taarifa kutoka Lisbon zasema mkutano wa pili kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiafrika umeidhinisha hii leo mpango wa kujenga uhusiano wa pande mbili zilizo sawa baina ya mabara haya 2.Viongozi hao wakitazamiwa kumaliza mkutano wao leo kwa kuafikiana juu ya mkakati wa ushirikiano kwenye maswali ya uhamiaji,biashara,nishati,mabadiliko ya hali ya hewa n a maendeleo.Isitoshe, UU unapanga kuvipa vikosi vya kuhifadhi amani barani Afrika msaada zaidi wa fedha.

Nchi za kiafrika kwa upande wao nazo, zinatakiwa kuchukua jukumu la kuheshimu haki za binadamu.

Taarifa kandoni mwa duru za mkutano mjini Lisbon, zasema pande hizo mbili zimeshindwa kuelewana juu ya mapatano mapya ya biashara kati ya mabara yao 2. Rais Abdoulaye Wade wa Senegal,amesema sehemu kubwa ya viongozi wa Afrika wanapinga mapendkezo ya UU ya biashara huru-EPA.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,

alimlaumu rais Mugabe wa Zimbabwe, kuharibu jina la bara la Afrika kwa kukanyaga nchini mwake haki za binadamu. Alisema,

1.O-ton Angela Merkel…………………………………

„Wakati unapita na hali za wananchi zazidi kuwa mbaya.

Labda huu ni mchango mdogo tu ikiwa mabadiliko huko yatatokea haraka.“

Jumuiya ya SADC ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kusini mwa Afrika imeutuhumu Umoja wa Ulaya kuuingiza mzozo wa Zimbabwe katika ajenda ya mkutano huu wa Lisbon.SADC inadai ,mada ya Zimbabwe haikuwamo katika ajenda iliokubaliwa na pande mbili.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ameususia mkutano wa Lisbon kutokana na kuhudhuria kwa rais Mugabe.

Kuhusu ushirikiano kati ya UA na UU rais wa Ghana John Koufour alisema:

O-Ton 2:

„Afrika inaihitaji Ulaya sawa na Ulaya inavyoihitaji Afrika.“

LISBON

Katibu mkuu wa zamani wa UM Kofi Annan, ameitisha „mapinduzi ya kilimo“ barani Afrika yakiiingiza ushirika baina ya serikali za Afrika na wakulima ili kuondosha njaa katika bara hili masikini.Annan alisema hayo kandoni mwa mkutano wa kilele wa Afrika na Ulaya mjini Lisbon jana.

Hapo kabla, waziri mkuu wa Spain Jose Luis Zapatero, alipendekeza mkataba kati ya UA na UU kupambana na uhamiaji usio halali.Zapatero alisema mapatano ya aina hiyo yalenge kukuza elimu,nafasi za kazi na kujenga miundo mbinu katika nchi zenyewe za Afrika wanakotoka wahamiaji hao.

BAGHDAD:

Bomu lililotegwa barabarani limemua leo mkuu wa polisi wa mkoa wa Babel kusini mwa mji mkuu Baghdad.Meja-jenerali al-Mamouri aliuwawa pale bomu liliporipuka katika mlolongo wake wa magari karibu na mji mkuu wa mkoa huo -Hilla.Polisi imearifu kwamba hata walinzi wake 2 wameuwawa na wengine 6 wamejeruhiwa.Mamouri akisifiwa mno na makamanda wa kimarekani huko kwa hjuhudi tzake kuimarisha usalama katika mkoa wa Barbel.

Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani nchini Iraq, yaligundua hapo kabla kasha la pili kwa ukubwa la silaha lililowahi kuonekana mjini Baghdad.Hii ilifuatia taarifa waliopewa na kikosi kimoja cha kujitolea.

Katika shehena hiyo na kuna aina mbali mbali ya mabomu ya kuharibu vifaru, mabomu ya mkono pamoja na zana nyingi kabisa za kutengezea miripuko.

LONDON:

Mwalimu mngereza aliepitishiwa adhabu ya kifungo nchini Sudan kwa kumuita Dubu-bandia kwa jina la Muhammad ,amesema katika mahojiano hii leo na gazeti moja kuwa anajilaumu binafsi kwa misukosuko iliomfika.

Bibi Gillian Gibbons alikutikana na hatia kwa kuibughdhi dini ya kiislamu baada ya kuwaruhusu wanafunzi wake wenye umri wa miaka 6 kumuita dubu-bandia darasani mwao ‚Muhammad“.

TEHERAN:

Msemaji wa wizara ya nje ya Iran, leo amekanusha madai ya mashirika ya ujasusi ya kimarekani kuwa Iran ilikua na mradi wa kuunda silaha za kinuklia kabla ya mwaka 2003.

„Iran haikuwa na mradi wa silaha za kinuklia wakati wowote-sio kabla 2003 wala baadae na madai yoyote yasemayo hivyo hayana msingi wowote.“

Kutokana na ripoti ya mashirika 16 ya ujasusi ya Marekani kukanusha Iran haikuwa na mradi wa silaha za kinuklia baada ya 2003, Iran imeanza kudai kwamba nchi za magharibi zikome kutoa mashtaka yoyote ya aina hiyo dhidi ya Iran na haioni uhalali wowote wa kupitishwa azimio jengine la UM kudai iwekewe vikwazo vya fedha.

BERLIN:

Waziri wa ndani wa Ujerumani amelieleza Kamnisa la „scientology“ linaloendesha shughuli zake kinyume na katiba ya Ujerumani na kwamba Idara ya Usalama ya Ujerumani itaandaa habari zinazohitajika ili kulipiga marufuku humu nchini.Matamshi ya Bw. Wolfgang Schauble, yametoka baada ya mawaziri wa ndani wa mikoa 16 ya ujerumani kuafikiana kwa sauti moja ijumaa iliopita kuchukua hatua kama hizo kwa kanisa hilo la scientology ambalo limekuwa likichunguzwa kwa muda mrefu.

CANNBERA:

Serikali ya Australia imekanusha taarifa kuwa imejitolea kubakisha majeshi ya Australia nchini Afghanistan hadi 2010.australia imekanusha hayo kujibu ripoti kuwa serikali ya Holland imeliambia Bunge lake kuwa Australia itajiunga na nchi nyengine kubakisha vikosi vyake nchini Afghanistan hadi wakati huo.

Waziri wa ulinzi wa Australia Joel Fitzgibbon amesema hakuna uamuzi uliokatwa kurefusha muda wa vikosi vya australia nchini Afghanistan kupindukia august,mwakani.

NJAMENA:

Kundi kuu la waasi nchini Chad liliwapa pigo kali vikosi vya serikali,kimeitaka austria kuandaa mkutano wa amani-hii ni kwa muujibu wa gazeti la kila wiki la Austria-Profil lilivyoarifu.

Jamadari Brahim Djidda kutoka Umoja wa vikosi vinavyopigania demokrasi na maendeleo (UFDD) amemuandikia waziri wa ulinzi wa austria akiutaka Umoja wa Ulaya kuchangia mno kutatua mgogoro nchini Chad.

NDJAMENA:

Taarifa nyengine kutoka Ndjamena zasema:

Raia 6 wa kifaransa waliowekwa kizuizini nchini Chad wameanza mgomo wa kukataa kula chakula.Wanadai hatima yao imesahauliwa.Wafanyikazi hao wa shirika la misaada ya kiutu Zoe’s Ark wanadai wana hisia serikali ya Ufaransa imewaacha mkono.

Wafaransa hao , wametuhumiwa kujaribu kuwakimbiza hadi watoto wadogo 100 kinyume na sharia kutoka Chad ili kulelewa nchini Ufaransa.

Shirika hilo wakati ule lilidai kwamba, wakidhani watoto hao walitoka Dafur, nchini Sudan- mkoa uliokumbwa na maafa ya vita.UM lakini uliarifu wengi wao wametoka vijiji vya nchini Chad.Tarehe ya kufunguliwa mashtaka wafaransa hao 6 bado haikuwekwa.

MWISHOE:MICHEZO:

Bayern Munich wamebakia kileleni mwa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani licha ya kwamba jana walimudu sare tu 0:0 na chipukizi Duisburg.katika mapambano mengine Bremen inayonyatia nafasi ya pili kileleni ililazwa na hannover 4-3 huku hamburg ikitoka nayo suluhu 0:0 na Cottbus.Mabingwa watetezi Stuttgart waliizaba Wolfsburg 3:1.

Katika ringi ya mabondia:

FLOYD Mayweather Jr, ametetea taji lake la wezani wa Welterweight la ubingwa wa dunia la shirika la WBC.Huko Las Vegas, alimdengua mapema alfajiri ya leo muingereza Ricky Hatton katika duru ya 10 kufuatia makonde ya mchanganyiko kutoka kulia na kushoto.Mara 2 Hatton aliporomoka chini.