1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneta Barack Obama ashinda jimbo la South Carolina

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyJE

WASHINGTON: Nchini Marekani, Seneta Barack Obama wa chama cha Democratic ameshinda katika kinyanganyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika jimbo la South Carolina.Obama amejisombea asilimia 55 ya kura kulinganishwa na Hillary Clinton aliejinyakulia asilimia 27 na hivyo kuwa mbele ya John Edwards aliepata asilimia 18 tu.

Katika hotuba yake ya ushindi,Obama alisisitiza kuwa ukabila hauna umuhimu katika uchaguzi.Amesema,chama cha Democratic kina msimamo mmoja,nao ni kukomesha kile alichokiita "sera za maafa" za serikali ya Bush.

Ushindi aliopata katika jimbo la South Carolina ulikuwa muhimu sana kwa Obama ili kuweza kubakia katika kinyanganyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic,baada ya Clinton kujinyukulia ushindi katika majimbo ya Nevada na New Hampshire.