1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sensa ya wafanyakazi wa serikali yafanyika nchini DRC

4 Aprili 2013

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imefahamu idadi ya wafanyakazi wa idara za umma nchini humo.

https://p.dw.com/p/189O4
Mji Mkuu wa Kinshasa, Jamhuri wa Kidemokrasi ya Kongo
Mji Mkuu wa Kinshasa, Jamhuri wa Kidemokrasi ya KongoPicha: Creative Commons/Moyogo

Kampeni ya sensa ya wafanyakazi wa serikali iliodhaminiwa na Afrika ya kusini imemalizika nchini humo. Serikali ya Kongo imeelezea kwamba ilikuwa ikipoteza kila mara dola milioni 20 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa, baada ya kubadili mfumo wa malipo ambao hivi sasa unafanyika kupitia benki. Kwa sasa jumla ya wafanyakazi ni laki tatu na hamsini elfu, zaidi ya nusu miongoni mwao wakiwa wazee. Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo na ripoti kamili. Kuskiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Josephat Charo