1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOL:Korea Kusini yalalani kuuawa kwa mateka wake mmoja

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfD

Korea ya Kusini imelaani mauaji ya mmoja wa mateka 23 raia wa nchi hiyo wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Taleban nchini Afghanistan.

Polisi nchini Afghanistan hapo jana waliuokota mwili wa mateka huyo, ambapo wateka nyara hao wametishia kuwaua wengine iwapo madai ya kuachiwa kwa wenzao wanaoshikiliwa na serikali ya Afghanistan hayatatekelezwa.

Mateka huyo mwanamume ni miongoni mwa mateka 23 raia wa Korea Kusini ambao wanashikiliwa na wanamgambo wa Taleban toka wiki iliyopita.

Hakuna uthibitisho rasmi juu ya taarifa za awali ya kwamba mateka wanane wakiwemo wanawake sita na wanaume wawili wameachiwa huru na kukabidhiwa jeshi la Marekani katika jimbo la Ghazni.

Kundi la Taleban limesema kuwa limemuua mateka huyo kutokana na serikali ya Afghanistan kushindwa kutimiza masharti yao.Hata hivyo afisa mmoja wa jimbo la Ghazni wanakoshikiliwa amesema kuwa mateka huyo alikuwa ni mgonjwa.

Katika tukio lingine mwandishi wa habari wa Denmark ambaye alitekwa nyara pamoja na mkalimani wake huko huko Afghanistan ameachiwa huru.

Wakati huo huo mwili wa mateka injinia wa kijerumani ambao uliokotwa Jumapili iliyopita umewasili nchini hapa.Bado majaaliwa ya mateka mwingine wa kijerumani anayeshikiliwa na wanamgambo wa Kitaleban hayajulikani.