1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul. Hali ya mawasiliano inakuwa bora.

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCff

Mawasiliano ya simu katika eneo la Asia yanarejea taratibu katika hali ya kawaida baada ya tetemeko la ardhi katika eneo la pwani ya Taiwan kuharibu waya na kuwaacha maelfu kadha ya watu bila mawasiliano ya mtandao wa internet.

Kiasi kikubwa cha huduma za simu katika eneo la Asia pamoja na Internet zimerejea lakini katika baadhi ya sehemu za Korea ya kusini na Taiwan bado hali si nzuri.

Kampuni kubwa linaloendesha huduma za simu na Internet nchini Korea ya kusini KT, pamoja na makamuni mengine ya eneo hilo yameonya kuwa itachukua wiki kadha kuweza kurejesha huduma zote.

Tetemeko hilo lililokuwa katika kipimo cha 7.1 katika kipimo cha Richter kililikumba eneo la pwani ya kusini mwa Taiwan siku ya Jumanne, na kuuwa watu wawili.