1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL: Maiti ya mateka wa Korea yawasili nyumbani

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdd

Maiti ya mchungaji aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan imewasili nchini Korea Kusini hii leo.

Jamii na marafiki walikusanyika kwenye kanisa la Saemmul mjini Bundang nje ya mji mkuu Seoul kotoa heshima zao za mwisho. Lakini familia yake imesema itachelewesha mazishi ya mchungaji huyo hadi mateka wengine 22 wa Korea Kusini wanaozuiliwa na kundi la Taliban nchini Afghanistan waachiliwe huru.

Kundi hilo limeirefushia muda serikali ya mjini Kabul hadi saa kumi jioni kwa saa za Afghanistan, iwaachie wafungwa wa kitaliban kabla kuanza kuwaua mateka hao.

Rais wa Korea Kusini Roh Moo- hyun amefanya kikao cha dharura leo mjini Seoul na kuwaamuru maafisa wake waongeze juhudi za kuwaokoa mateka wote 22.

Rais huyo pia amemuamuru mshauri wake mkuu aliye hivi sasa nchini Afghanistan, aendelee kubakia nchini humo kwa siku kadhaa zaidi ili kuziongezea nguvu juhudi za kuwakoa mateka hao.