1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL : Viongozi wa Korea wajizatiti kwa amani

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IQ

Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini hapo jana wametowa wito wa kuwepo kwa bara la Korea lisilokuwa na silaha za nuklea na mkataba wa amani wa kudumu kukomesha Vita Baridi vya mwisho kati ya nchi hizo.

Mahasimu hao wa kihistoria wamekubali kuimarisha biashara kati yao,usafiri na ziara za kisiasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha treni ya mizigo kati ya nchi hizo mbili pamoja na usafiri wa ndege kwa idadi inayoongezeka ya wataalii wa Korea Kusini.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Il na Rais Roh Moo-Hyun ambaye anakuwa rais wa pili wa Korea Kusini kuitembelea Korea Kaskazini wameufunga mkutano wao wa siku tatu kwa kusaini makubaliano yenye kuahidi kushirikiana katika kufikia amani ya kudumu baina ya nchi hizo.